Monday, January 31, 2011

KONGAMANO LA VIONGOZI WA VIJANA (VIWAWA)JIMBO KUU ARUSHA.

Viongozi wa maparokia yote ya jimbo kuu la Arusha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa misa kongamano la viongozi  lililoanza tarehe 28/1/2011 - 30/1/2011. Kikao hicho kilifanyika parokia ya moyo safi Unga LTD Kituo cha malezi. Mada kadhaa za  kuwaandaa viongozi kwa mwaka huu wa kongamano la kitaifa litakalo fanyika jimboni Arusha. yafuatayo yalijadiliwa kwenye kikao hicho ambacho ki-utaratibu kilifahamika kama kikao cha halmashauri ya vijana (VIWAWA) Jimbo kuu la Arusha. viongozi wa jimbo waalisoma  muhtasari  wa mkutano, yatokanayo,walisoma taarifa ya utekelezaji,walisoma taarifa ya fedha, Kujadili kongamano la taifa + dunia  na kuweka maazimio.  Mengi yaliyojadiliwa  pamoja na mipango pia yanahitaji zaidi maombi na sala ili yaweze kufanikishwa, kila mmoja wetu anapopanga jambo basi amtangulize Mungu. Mungu aibariki Halmashauri ya Jimbo kuu  la Arusha na mafanikio mema. ya maandalizi aaaaamen.   Mwandishi. Majegero Selecius.

Kanisa Katoliki...

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rukia: urambazaji, tafuta
Papa Benedikto XVI, askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani
Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo
Papa: Benedikto XVI
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki
Historia
Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi
Ibada
Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi
Mapokeo ya liturujia
Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Lyon Toledo)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia
Jina hilo linatumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya Papa wa Roma kama mkuu wa Maaskofu juu yake lote.
Kanisa hilo linaamini kuwa ndani yake linadumu moja kwa moja Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu Kristo ambalo wanaunganishwa nalo wote wanaobatizwa katika madhehebu yoyote. Tofauti kati yao ni kwamba baadhi (Wakatoliki) wana ushirika kamili nalo, wakati wengine (hasa Waorthodoksi na Waprotestanti) wana ushirika nalo la viwango mbalimbali, kadiri wanavyokubali mafundisho, sakramenti na uongozi wake.
Neno "katoliki" linatokana na kivumishi cha Kigiriki καθολικός (katholikòs), lenye maana ya «kamili, kadiri ya utimilifu». Kwa mara ya kwanza liliandikwa na Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wa Smirna mwanzoni mwa karne II: «Alipo Yesu Kristo ndipo lilipo Kanisa Katoliki» (Ad Smyrnaeos, 8).
Kati ya madhehebu ya Kikristo, Kanisa Katoliki linakusanya waamini 1,147,000,000, yaani nusu ya wafuasi wote wa Yesu, na 17.3 % ya binadamu wote, likiwa na asilimia kubwa ya waamini kati ya wananchi wa Amerika na Ulaya.
Kanisa Katoliki linaishi katika majimbo karibu 3,000, ambayo kwa kawaida yanaongozwa na Maaskofu wakisaidiwa na mapadri na mashemasi; kati ya hayo, mengi yanafuata mapokeo ya magharibi, lakini machache mapokeo ya mashariki. Majimbo yanagawanyika katika parokia zinazoongozwa na padri anayeitwa paroko.
Kati ya waamini wana nafasi ya pekee wamonaki na watawa wengine ambao wanaishi kwa mitindo iliyostawi katika historia ya Kanisa ili kumfuata Yesu kwa karibu zaidi katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu.

MOTO WA KATIBA MPYA WAZIDI KUSHIKA KASI, KANISA KATOLIKI WAJITOSA

HATIMAYE Kanisa Katoliki nchini limejitosa rasmi katika mjadala wa katiba mpya likisema kuwa linaunga mkono mchakato huo, lakini likihadharisha kuwa mchakato huo unahitaji subira, weledi na ujasiri wa kisiasa kukubali mabadiliko.

Hayo yamo katika tamko maalumu lililotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) katika mkutano usiokuwa wa kawaida uliofanyika jijini Mwanza kuanzia Januari 10-11, mwaka huu na  kusainiwa na Rais wa baraza hilo Jude Thaddaus Ruwa’ichi.

Maaskofu wa kanisa hilo pamoja na mambo mengine walizungumzia suala la katiba mpya na tukio la kitaifa la maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wa nchi.

Kanisa hilo lilitoa wito kwa serikali na wadau wote kujadili mchakato huo wa kuandika katiba mpya likitaka busara itumike ili kufuata mchakato uliowazi wakati wa kuiandaa.

“Tunamshukuru, kwanza Rais amelitambua hilo na hivyo amekubali na kudhamiria kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa na utaratibu mzuri wa kuratibu mambo yake kwa njia ya katiba inayoendana na wakati,” lilisema kanisa hilo kupitia tamko hilo maalumu na kuongeza.

“Ni matarajio yetu kwamba ili kufikia lengo na matamanio ya Watanzania walio wengi ya kuwa na katiba inayoendana na wakati, yenye misingi imara ya kidemokrasia na inayobeba matumaini ya Watanzania kuelekea miaka 50 ijayo, busara itatumika ili kufuata mchakato uliowazi.”

Kanisa lilifafanua kuwa katika kutumia busara huko kutafanya mchakato huo kuwa wazi wa  haki na unaokubalika na wengi na kwamba utawezesha  kupatikana kwa  katiba inayolinda tunu za taifa ambazo ni amani umoja mshikamano  na pia maslahi ya Watanzania wote.

Kanisa limeshauri uwapo wa jitihada za makusudi za kushirikisha watu wengi kutoka makundi mbalimbali yatakayochangia kupata mwafaka wa kitaifa juu ya katiba gani wanayoitaka Watanzania.

“Kwa kuwa bunge ni chombo cha wawakilishi wa nchini vema chombo hiki kikishirikishwa tangu mwanzo hasa katika kuweka taratibu za kufanikisha shughuli hiyo na mwisho kupata ridhaa kwa wananchi wote (referendum), mchakato huu utahitaji weledi, subira, uvumilivu wa kisiasa na ujasili wa kukubali mabadiliko,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika tarifa hiyo maaskofu waliweka bayana kuwa wao wanaunga mkono na kwamba wanatia moyo mchakato huo na na kuwaalika Watanzania wote kuungana pamoja kuliombea taifa liweze kudumu katika upendo uelewano umoja na amani.

Kuhusu maadhimisho ya Jubilie ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kanisa limeelekeza waumini wake kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo kwa kusali sala maalumu ya kuliombea taifa kuanzia ngazi ya Jumuiya, Parokia na Jimbo.

“Wazo  ama lengo kuu la Kanisa Katoliki kusherehekea Jubilei ya Uhuru wa Tanzania ni kumshukuru Mungu na kuona kwamba uhuru tulioupata unaendelea kuwasaidia watu kuishi kama wana wa Mungu, maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania pia yamelenga kuongeza uelewa wa waumini na Watanzania wote juu ya umuhimu wa uhuru wa watu na taifa,” lilisema.

Sababu nyingine ni kutathmini mafanikio, matatizo, na changamoto muhimu za kitaifa za kanisa katoliki katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru katika kumwendeleza  Mtanzania kiroho na kimwili na kuweka malengo ya jumla ya kudumisha uhuru wa Taifa la Tanzania.

Katika kuhakikisha kanisa linashiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo, limeziagiza mamlaka zake za chini kuanzia ngazi ya jumuiya, kigango na Parokia kusali sala maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara kila zinapokutana na kuimba wimbo wa taifa pale inapobidi kufanya hivyo.

“Ili kufanikisha hilo, pamoja na mambo mengine , tunapendekeza kwamba kadiri ya nafasi na mazingira, wimbo wetu wa Taifa uimbwe mara kwa mara kadiri iwezekanavyo katika ibada zetu kama vile katika misa za Jumapili na katika shughuli zingine za kikanisa”, lilisema tamko.

Pia imeelezwa kuwa Parokia na Jimbo zitatakiwa  kutenga siku maalum kwa ajili ya kuadhimisha misa maalumu kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 50 ya uhuru na kuliombea Taifa liweze kudumu katika upendo, amani umoja na mshikamano.

“Misa hizi ziadhimishwe kwa kufuata mtiririko kulingana na Kalenda ya litrujia, iteuliwe siku moja kwa ajili ya Misa ya Parokia, misa hii ifanyike Mei 31 na Agosti 15 , Misa ya Jimbo na ile ya kitaifa itafanyika karibu na kilele cha Sherehe za Uhuru  (Desemba 9  mwaka huu,” lilisema kanisa hilo.

Kanisa  hilo lilifafanua kuwa katika sherehe hizo kutakuwa na harakati za kuwahamasisha Wakristo na Watanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa uhuru katika kujipatia maendeleo ya kiroho na kimwili.

Aidha kanisa hilo  limeitisha kongomano la kitaifa litakalofanyika Novemba 11 na 12 mwaka huu, lengo likiwa kutoa fursa kwa waumini na watu wote kutafakari juu ya wapi wametoka, walipo na wanakotaka kwenda kama taifa.

Moto wa kudai katiba mpya, uliwashwa na Chadema Novemba mwaka jana, baada ya kutangaza kutotambua kura zilizomweka madarakani Rais Jakaya  Kikwete. Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilianza mchakato wa kushikiza kuundwa kwa katiba mpya kwa kususia hotuba ya Rais Kikwete wakati wa akizindua Bunge la 10.

Pia wabunge pamoja na viongozi wa chama hicho walisusia sherehe za kuapishwa kwa Rais.
Katika kuendeleza madai hayo, hivi karibuni mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chadema, John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kwenye Ofisi za Bunge, hoja iliyokuwa na lengo la kudai katiba mpya.

Nao Wanachama wa CUF,  hivi karibuni walifanya maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya kwa Waziri wa Katiba na Sheria. Pia viongozi mbalimbali wastaafu, walipo madarakani wamekuwa wakieleza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

Miongoni mwa waliojitokeza adharani na kuunga mkono uwepo wa katiba mpya ni pamoja na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mawaziri Wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye, Jaji Mkuu Mstaafu na Augustino Ramadhani, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye aliahidi kumshauri Rais juu ya suala la kuundwa kwa Katiba mpya.

Madai ya Katiba mpya pia yamewahi kutolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya, akitoa mfano wa mapungufu ya katiba ya sasa kuwa ni rais kupewa madaraka makubwa.

Lakini akiwa Ikulu kwenye hafla ya kuapishwa Jaji Mkuu Mpya, Mohamed Othman Chande, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Frederick Werema, alisema kuwa haoni haja ya kuandikwa katiba mpya badala yake katiba iliyopo, iwekewe viraka.

“Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa,” alisema Jaji Werema.