Maana ya Viwawa

MAANA YA VIWAWA NA HISTORIA YA VIWAWA .
MAANA YA VIWAWA.
Viwawa maana ya Viwawa ni Vijana Wakristo Wakatoliki(Wengine wanasema ni Vijana Wakatoliki Wafanyakazi) Viwawa ni chama cha kitume cha Vijana ndani ya Kanisa ambao wanatumwa na Yesu mwenyewe kuendelea  kazi yake kwa watuwake kwamba yeye “NDIYE NJIA YA KWELI NA UZIMA”Kwa Vijana wote katika maisha yao ya kila siku.

HISTORIA YA VIWAWA KIDUNIA.
Viwawa ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgijina Padri Joseph Cardjin na kupitishwarasimi na kama chama cha kitume cha vijana Kimataifa na Balaza la Kipapa Vatican mwaka 1950.Padri Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA Na YCS alianzisha yeye.Makao makuu ya VIWAWA Duniani yako Roma-Italia chini ya Rais Seraphina kutoka Korea,Katibu Mkuu Jules Adached toka Bejin,Mhazini Lisa Vaccariano toka Italia na Mratibu wa kimataifa Arniel Iway toka Philipini na mshauri Pd.Joseph Ramaguera toka Spain. 

 HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA.
Viwawa Tanzania iliingia mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi,Jimbo kuu la Dar es salaam chini ya Mwanzilishi Padri Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Padri Mansuetus na kupitisha rasimi chama cha Kitume cha Vijana na Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) mwaka 1979.Baada ya kupitisha hapo kilitambulishwa pote Tanzania kama chama cha Vijana Wakatoriki Wafanyakazi Tanzania(VIWAWA).
Mpaka sasa chama hiki kipo kipo majimboni,kuanzia ngazi ya Jumuiya,Mtaa,Kanda,Kigango,Parokia,Kijimbo,Taifa na Kimataifa.

LENGO LA CHAMA.
Ø      Kumuezesha Kijana awe mkristo wa kweli na raia wengine waweze kurekebisha,Kuendeleza na Kudumisha taratibu za uchumi,utamaduni,ustawi,siasa na utaalamu kufatana na mpango wa Mungukatika kutafakali injili na kusali.

Ø      Kuunda umoja na ushirikiano kwa vijana kadili ya injili na mafundisho ya Yesu Kristo.

Ø      Kuishi upendo wa Kikristo kama watoto wa Baba mmoja.Hii ni amri ya Yesu “Amri mpya nawapa pendaneni kama vilenilivyowapenda ninyi,nanyi mpendane vivyo hivyo.(Yoh 13:34-35).